Ni jambo la busara kwa mwalimu kuvifanyia vielelezo/zana majaribio kabla ya kuvitumia.
Hatua hii humwezesha kufanya yafuatayo:-
a) Kuona kama zana/ vifaa ni vizima au ni vibovu viweze kutengenezwa/ kununua/ kutafuta vingine.
b) Kuhakikisha kama zana/ vifaa hivyo vinafanya kazi kwa usahihi kama vilivyokusudiwa
c) Kujiamini katika kufundisha hatua anuai za somo lake na kutumia vielelezo vyake
d) Kujua uthabiti na udhaifu wa vielelezo vyenyewe
e) Kuhakikisha kwamba havijaharibika, na kama vimeharibika aweze kuandaa vingine kabla ya siku ya somo lenyewe
f) Kufahamu madhara yanayoweza kuletwa na vielelezo hivyo mfano:- Tindikali n.k.
g) Kufahamu namna ya kutumia vielelezo hivyo.
JIUNGE NA CHUO CHA UALIMU AGGREY-MBEYA
0 maoni:
Chapisha Maoni