DHANA YA KKK
Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ni msingi katika kujifunza ujuzi na maarifa yote yatolewayo kwa njia ya maandishi.
Mtu yeyote anayekusudia kupata ujuzi na maarifa ya masomo mbalimbali kupitia mfumo rasmi shuleni, inampasa ajifunze na kuelewa vema KKK.
Dhana ya KKK inapatikana katika masomo yote ambayo yanawasilishwa kwa maandishi.
Watu wengi hufikiri kuwa KKK hufundishwa na inastahili kufundishwa katika masomo ya lugha hasa Kiswahili na English tu, hii si kweli kwa sababu masomo yote hueleweka kwa mlengwa baada ya kupata stadi za KKK.
Ungana nasi katika sehemu ya pili ya Makala hii upate ufahamu zaidi kupitia swali linalouliza;
Je, kuna umuhimu gani kufundisha KKK katika masomo mengine?
0 maoni:
Chapisha Maoni